Dkt. Sheikh Reyhan: "Ziara ya Arobaini ya Imam Hussein (a.s) si ibada ya kimwili pekee, bali ni ahadi ya kudumu katika kushikamana na malengo ya Kihusseini na kusimama dhidi ya dhulma na batili".
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-
Kwa mujibu wa taarifa, maadhimisho ya siku ya Arobaini ya Imam Hussein (a.s) yamefanyika Leo hii (15-08-2025) katika Msikiti (Muswalla) wa Jamiat al-Mustafa (s) Jijini Dar es Salaam - Tanzania.
Khatibu wa Majlis hii alikuwa ni: Dkt. Sheikh Reyhan Yasin, ambapo alizungumzia mada muhimu kuhusiana na Fadhila za Ziara ya Arobaini ya Imam Hussein (a.s), akibainisha nafasi ya juu ya ziara hii katika mafundisho ya Kiislamu na umuhimu wake katika kuimarisha imani, kusimama imara katika njia ya Haki, na kudumisha uhusiano na maadili ya Harakati ya A'shura.

Amesisitiza kuwa Ziara ya Imam Hussein (as) si ibada ya kimwili pekee, bali ni ahadi ya upya ya kushikamana na malengo ya Kihusseini na kusimama dhidi ya dhulma na batili.
Your Comment